Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, April 9, 2014

Wadau wa filamu waaswa kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa.

Baadhi ya wadau wa filamu walioshiriki kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya husuyo tasnia hiyo leo jijini Dar es salaam. Pichani ni wasanii wa “Bongo Movie” (wa kwanza kushoto ni Steven Mengele “Manyerere”, Emmanuel Muyamba (katikati) na Jacobo Steven “JB”(wa kwanza kulia)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha wadau wa filamu kuhusu mstakabali wa soko la filamu nchini leo jijini Dar es salaam.

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bi Joyce Fisoo akieleza lengo la kikao cha wadau wa filamu ni pamoja na kujadili masuala ya maendeleo ya tasnia ya filamu nchini na mapendekezo ya wadau kuhusu bodi ya filamu kuitisha mjadala wa wazi wa wadau wa filamu hususani wasambazaji, waandishi wa miswada na watayarishaji ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia hiyo leo jijini Dar es salaam.

Na Eleuteri Mangi
Wadau wa filamu nchini waaswa kuendelea kupeperusha vizuri zaidi bendera ya Tanzania katika tasnia hiyo na kuiweka kwenye ramani ya dunia.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa filamu kuhusu mstakabali wa soko la filamu nchini leo jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu Bi. Sihaba alisema kuwa kikao hicho ni fursa pekee kwa wadau hao kuweka mikakati ya kuiendeleza tasnia ya filamu nchini hususani suala zima la mustakabali wa soko la filamu.

“Ni matumaini yangu maazimio yatakayotokana na mjadala wenu yatakuwa ya manufaa kwa tasnia nzima na yataiwezesha Serikali kutoa mwongozo, ikiwemo suala la bei elekezi ili bidhaa za filamu ziwe na mfumo wa bei ambao utazinufaisha pande zote mbili” alisema Bi. Sihaba

Aidha, Katibu Mkuu Bi. Sihaba alisema kuwa ni vizuri filamu zinazotengenezwa nchini ziwe zinabeba maisha halisia ya Kitanzania ili kutangaza nchi yetu na fursa zilizopo ndani na nje ya nchi.

Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bi Joyce Fisoo alisema kuwa lengo la kikao hicho na wadau wa filamu kinaongozwa na sababu kuu nne ikwemo kujadili masuala ya maendeleo ya tasnia ya filamu nchini na mapendekezo ya wadau kuhusu bodi ya filamu kuitisha mjadala wa wazi wa wadau wa filamu hususani wasambazaji, waandishi wa miswada na watayarishaji ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia hiyo. Malengo mengine ni nia ya wadau kuanza kuuza filamu kwa mkusanyiko kitu ambacho ni kigeni kwa soko la filamu za Kitanzania na mapendekezo ya bei ya mkusanyiko wa filamu kuwa sh. 2000 kila moja ili Serikali iweze kutoa mwongozo wa suala hili.

Pia kujadili suala la ubora wa kazi za filamu ikibeba maudhui yanayojali na kuzingatia maadili ya kitanzania na namna zinavyohifadhiwa kwa nia ya kupelekwa sokoni.

Kwa upande wake Meneja wa Masoko kampuni ya Harmony Entertainment Waziri Msangi kwa niaba ya wajumbe wa kikao alimshukuru Katibu Mkuu Bi. Sihaba kwa kufungua kikao hicho na kuahidi kuwa wadau wa tasnia ya filamu nchini wataendelea kuelimisha, kuonya na kuburudisha jamii kupitia kazi wanazotoa kwa kuzingatia maadili ya kazi yao na maadili ya Kitanzania.

Wadau walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Filamu, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Prof.Hermans Mwansoko, mwakilishi wa Shirika la Viwango vya Ubora Tanzania, wawakilishi kutoka TRA, COSOTA na BASATA Bodi ya Filamu na wasanii mbalimbali wa “Bongo Movie” akiwemo Ahmed Olotu “Mzee Chilo”, Jacobo Steven “JB” na Steven Mengele “Manyerere”.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment