Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kushoto) akitoa risala siku moja kabla ya ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze kwa waadishi wa habari leo katika ukumbi halmashauri ya mji wa Bagamoyo. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Hamid Mahmuod na wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Tume hiyo Prof. Amon Chaligha.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo wakati kisoma risala siku moja kabla ya siku ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze kwa waadishi wa habari leo katika ukumbi halmashauri ya mji wa Bagamoyo. Na wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Tume hiyo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki John Joseph Mkwawa.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) wakati kisoma risala siku moja kabla ya siku ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze kwa waadishi wa habari leo katika ukumbi halmashauri ya mji wa Bagamoyo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati akisoma risala siku moja kabla ya siku ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze ikiwa ni utaratibu uliwekwa na tume hiyo kabla ya uchaguzi. Picha zote na Eleuteri Mangi.
Na Eleuteri Mangi
Wapiga kura wote waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo la Chalinze wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili wamchagua kiongozi wao wanaomtaka.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva alipokuwa akitoa risala kwa waadishi wa habari leo katika ukumbi halmashauri ya mji wa Bagamoyo siku moja kabla ya siku ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Chalinze.
Mwenyekiti huyo Jaji Mstaafu Lubuva alitoa wito kwa waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi huo wajitokeze kwa wingi na kwenda kwenye vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kupiga kura nakwa hatua hiyo watakuwa wemetekeleza haki yao ya kikatiba ya kumchagua mtu wanayempenda kuwa kiongozi wao.
Ili kuhakikisha uchaguzi umekuwa wa haki ha amani, Jaji Mstaafu Lubuva alisisitiza kuwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze vinatakiwa kuhakikisha vinaweka mawakala wake katika vituo vyote vya kupigia kura, kuhesabia na kujumlisha kura.
Aidha, mawakala hao watatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwemo kutokuandika majina ya wapiga kura na namba zao za kadi.
Vile vile Jaji Mstaafu Lubuva alisisitiza kuwa upigaji kura ni wa siri, hivyo kila mtu apige kura yake kwa siri na asishawishiwe na mtu yeyote kueleza nani amaempigia kura, ikumbukwe kuwa kura ni siri ya mpiga kura.
Zaidi ya hayo, Jaji Mstaafu Lubuva alisema kuwa mpiga kura anayeishi na ulemavu wa kutoona au asiyejua kusoma na kuandika ataruhusiwa kuja kituoni aliyemchagua yeye mwenyewe.
Kwa kuzingatia sheria mtu mmoja anaweza kumsaidia mpiga kura mmoja tu, labda kama wapo wapiga kura zaidi ya mmoja kutoka familia moja.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi alisema kuwa mara baada ya kupiga kura na kuzingatia maadili ya uchaguzi, wapiga kura wanatakiwa kuondoka vituoni na kurejea nyumbani kwa kuwa vyama vya siasa vitakuwa vimeweka mawakala wake ambao watalinda maslahi ya vyama husika na wagombea wao.

Risala hiyo ya Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni utaratibu uliowekwa na tume hiyo kuongea na vyombo vya habari ili kuwahabarisha wananchi wa eneo husika la uchaguzi na taifa kwa ujumla siku moja kabla ya tarehe ya uchaguzi ambapo kwa jimbo la Chalize uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo hilo utakuwa ni Aprili 6, mwaka huu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmedi Kipozi amewahkikishia wananchi wa Chalinze na Bagamoyo kwa ujumla kuwa kutakuwa na ulinzi wa kutosha katika wilaya yake na vituo na wapiga kura watapiga kura zao kwa amani na utulivu pasipobughudha wala vitisho vya aina yeyote.
Katika uchaguzi huo jimboni Chalinze, vyama vitano vimewasimamisha washiriki wao katika kumtafuta mwakilishi wa wananchi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, NRA na AFP.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment