Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, April 8, 2014

STEPS SOLAR KUSAIDIA KUFUNGA SOLAR BURE MASHULE, HOSPITALI VITUO VYA POLISI, DAR ES SALAAM.

Selles Mapunda Meneja masoko Steps Solar

APRIL, 2014 TAREA – Ubungo Extenal, Dar es Salaam.

Kampuni ya Steps Solar Ltd inatarajia kutoa msaada katika Mashule, Zahanati, pamoja na vituo vya Polisi ikiwa ni moja katika harakati za kuhakikisha Tanzania inakuwa katika Nuru, kampuni kwa kuona umuhimu wa huduma katika jamii imelenga kuitambulisha steps Solar kwa sehemu nyeti zilizotajwa hapo juu,Steps Solar ni kampuni dada ya Steps Entertainment Ltd.

Steps Solar ilianzishwa na Bwana Solanki mwaka 2013, lengo ikiwa kuwaongezea masla hi wasanii wa filamu ambao wamekuwa wakifanya kazi na Steps Entertainment Ltd, Steps Solar ina mabalozi wake ambao ni mabalozi wa bidhaa zake hizi, ambao ni Jacob Stephen ‘JB’, Irene Uwoya, na Athuman Amri ‘King Majuto’.

Akiongea na waandishi wa habari afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Moses A. Mwanyilu amesema “ kutambua kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanaishi bila ya huduma ya umeme na gharama ya umeme pia kuwa kubwa Steps Solar imeamua kuwapatia watanzania umeme Nuru ulio wa uhakika na kwa bei rahisi sana, Vile vile kampuni ya Steps Solar bidhaa zake zina dhamana ya kati ya miaka miwili mpaka miaka ishirini na tano,”anasema Mwanyilu.

STEPS SOLAR pamoja na TAREA kwa pamoja wameamua kutoa na kufunga bure baadhi ya vifaa vyake kwenye vituo vya umma pamoja na baadhi ya taasisi za serikali kama vile SHULE ZA SEKONDARI (Kidete na Kibugumo) ZAHANATI (Kibugumo, Mji Mwema, Tuangoma, Homboza) Vituo vya Watoto Yatima (Ungindoni, Mji Mwema Miti Mirefu, Yatima Charity) Ofisi za Serikali (Mji Mwema na Feri) na Baadhi ya Vituo vya Polisi(Mji Mwema) katika kata za Mji Mwema na Chanika.

Zaidi ya kufunga mifumo ya umeme Nuru, Steps Solar na TAREA watafanya matamasha ya wazi katika vitongoji vya Mji Mwema na Homboza yatakayolenga kutoa Elimu ya umeme nuru kwa wananchi. Wakati wa matamasha zawadi za taa za umeme Nuru, fulana na kofia zitatolewa kwa watakao jibu vyema maswali ya ufahamu. Huduma hiyo itagharimu kati ya shilingi milioni 20 mpaka 30 fedha halali za Tanzania.

Na huduma hiyo itaanza tarehe tarehe 4/4/2014 na kufikia kikomo tarehe 19/4/2014. Steps Solar inawakumbusha watanzania kutohofia kununua bidhaa zake kwani ukiachilia mbali kuwepo na uhakika wa usalama na pia kuna mafundi walio na uzoefu wa hali ya juu Kumbuka ni jukumu letu sote kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele kwa maendeleo.

Steps Solar inahitaji kuweka mazingira ya Tanzania kuwa ya kijani zaidi.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment