Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.
Wasanii wa kikundi cha ngoma na maigizo cha kijiji cha Mahumbika, Lindi wakitoa burudani wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.
Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela akisoma hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila hivi karibuni.
Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (kushoto) akikabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila (kulia) na Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Absalom Bohela (kushoto) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mahumbika wakati wa kukabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa shule za mkoa wa Lindi hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu:
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imekabidhi msaada wa madawati 110 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa shule za Mkoa wa Lindi katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika kijiji cha Mahumbika kilichopo Lindi vijijini.
Msaada huo wa madawati umekabidhiwa kwa shule hizo hivi karibuni na mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Absolom Bohella mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwananzila.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Ludovick Mwanzila ameushukuru uongozi wa TPA kwa msaada huo na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa TPA katika kuchangia elimu ya Mkoa wa Lindi.
“Napenda niwashukuru Mamlaka ya Bandari kwa msaada huu lakini pia isiwe mwisho na niziombe taasisi nyingine ambazo tumeziandikia kuziomba madawati kujitokeza na kutimiza ahadi walizotupa ili wanafunzi wetu wapate mazingira mazuri ya kusomea,” amefafanua Mwanzila.
Kwa upande wake Bw. Bohella ambaye pia ni Mkuu wa Bandari ya Mtwara ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Lindi pamoja na ule wa Chuo cha Veta kwa ushirikiano walioutoa wakati wa ujenzi na usambazaji wa madawati hayo.
“Napenda kuishukuru Ofisi yako pamoja na uongozi wa Chuo cha Veta kwa kutupa ushirikiano mzuri wakati wa ujenzi wa madawati haya ambayo kwa kweli yametengenezwa kwa ubora wa hali ya juu jambo linalodhihirisha kuwa Veta wanaweza,” amefafanua Bohella.
Mbali na kutoa misaada kwa jamii, Bohella amekumbusha kwamba TPA inatambua na imejizatiti kutoa huduma zake kwa ufanisi na viwango vya hali ya juu ili kuinua pato la Mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla.
Amesema kwamba TPA kama zilivyo taasisi nyingine za Serikali zilizopo katika mpango wa ‘Matokeo Makubwa Sasa,’ inatekeleza majukumu yake kwa kasi na ufanisi.
Bohella amezipongeza shule zote ambazo zimenufaika na msaada wa madawati na kuwaasa viongozi wa shule pamoja na wanafunzi kuyatunza madawati waliyogaiwa ili yatumike na vizazi vingi vijavyo.
Imetolewa na:
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
Makao Makuu
Dar es Salaam
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment