Manchester United ya England jana usiku imeaga ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa mabao 3-1 na wenyeji Bayern Munich Uwanja wa Allianz-Arena mjini Munich, Ujerumani usiku huu. Hiyo inamaanisha United imeaga kwa kipigo cha jumla ya mabao 4-2, baada ya awali kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester.
United ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 57, mfungaji beki wake Mfaransa, Patrice Evra aliyefumua shuti kali kwa guu la kushoto baada ya kupokea pasi ya Antonio Valencia.
Katika mchezo mwingine, Barcelona imefungishwa virago na Atletico Madrid, zote za Hispania baada ya kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania. Hiyo inamaanisha Barca imeaga kwa kipigo cha jumla cha mabao 2-1 baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 Uwanja wa Camp Nou, Barcelona.
Bao lililoizamisha Barca limefungwa na Jorge Resurrecion Merodio Koke dakika ya tano akimalizia pasi ya Adrian.
Bayern na Atletico zinaungana na Chelsea ya England iliyoitoa PSG ya Ufaransa na Real Madrid ya Hispania iliyoing’oa Borrussia Dortmund jana kutinga Nusu Fainali, ambayo droo yake itapangwa Ijumaa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment