Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, July 3, 2019

CHAI BORA YAENDELEA KUUNGA MKONO KILIMO TANZANIA KUPITIA BIDHAA ZAO

Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Chai Bora Limited katika banda lao katika viwanja vya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Chai Bora imekaribisha wateja wanaotembelea maonesho ya saba saba kutembelea banda lao na kuonja bidhaa tofauti zikiwemo bidhaa za chai, kahawa na Dabaga.

Chai Bora ni wachanganyaji na wapakiaji wa aina za chai zinazokiji mahitaji ya makundi mbalimbali ya watumiaji nchini na nje ya nchi. Wakiwa na uzalishaji wa zaidi ya kilo Milioni 3.5 kwa mwaka, Chai Bora hutumia nguvukazi kutoka kwenye jamii zinazowazunguka na hivyo kutengeneza fursa za ajira katika jamii na katika mnyororo wa usambazaji wa bidhaa kote nchini.

“Tuna furaha kukaribisha Watanzania katika banda letu ili waonje bidhaa zetu. Katika jitihada za kuunga mkono kilimo, chai zetu zinatengenezwa kutokana na malighafi bora zinazozalishwa hapa nchini na pia tunachangia katika kutengeneza fursa za ajira. Tunatumia malighafi bora za kitanzania na ubunifu wa hali ya juu. Na kupitia ubunifu huu, tunafurahi kuwa washindi wa kwanza katika kipengele cha banda bora la bidhaa za chakula na vinywaji katika maonyesho haya” Alisema Awatif Bushiri, Meneja Masoko.

Majani ya chai ya Chai Bora yamekuwa yakitumika na watanzania kwa miaka mingi. Wakiwa na aina nyingi za majani, chai bora wanaendelea kuunga mkono wakulima huku wakiwapatia watumiaji bidhaa kulingana na mahitaji yao.

“Iwe ni majani ya kawaida au yale yaliyo katika vipakti vidogo, wateja wetu wanaweza kufurahia bidhaa zetu zikiwa katika mfumo wowote wanaopendelea.” Aliongezea Awatif

Chai Bora pia huuza bidhaa zao nje ya nchi katika nchi za Kenya, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu, Rwanda na Ghana. Katika kukuza usambazaji wa bidhaa nje ya nchi, Chai Bora imeshirikiana na TWIGA ALPHA kuzindua mfumo wa MDUKA ambao unaruhusu watumiaji popote duniani kufanya manunuzi ya Chai Bora kupitia mfumo huo.

Kuhusu Chai Bora Limited

Chai Bora ilianza shughuli zake mwaka 1994 kama nembo ya chai, na kusajiliwa kama kampuni ya Chai Bora Limited mwaka 2006. Chai Bora huchanganya na kufungasha bidhaa za ubora wa hali ya juu huku wakitengeneza fursa za ajira nchini Tanzania.

Mwaka 2015, Chai Bora ilichukua rasmi uendeshaji wa nembo ya DABAGA na kujenga kiwanda cha kisasa huko Ilula, Iringa. Pia, Chai Bora imetambulisha kahawa yake iitwayo CAFEBORA ambayo inapatikana kama kahawa ya unga na kahawa ya kusagwa.

Chai Bora ni nembo inayotambulika nchini ikiwa na kiwanda chake wilayani Mafinga ambapo ni kitovu cha kilimo cha chai nchini. Pia, Chai Bora inaongoza katika soko la chai kupitia bidhaa zake za chai zenye viwango vya ubora kimataifa – ISO 22000:2005.

Hivi karibuni, Chai Bora imeanza kufanya kazi chini ya kampuni ya Catalyst Principal Partners, na kampuni hiyo ina lengo la kuwa kinara katika biashara ya vinywaji nchini na kusini mwa Afrika.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment