Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, April 22, 2014

Serikali kuimarisha Masoko 18 jijini la Dar es Salaam

Afisa Uhusiano Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusu mpango wa serikali wa kuendelea kuimarisha Masoko katika Jiji la Dar es Salaam, Wakati wa Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko wa Manispaa hiyo Bw. Athuman Mbelwa. Picha na Fatma Salum

Na Frank Mvungi.
Serikali yaimarisha masoko 18 katika jiji la Dar es salaam katika kukabiliana na Ongezeko la Mahitaji ya Wananchi.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu wakati wa mkutano nawaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akifafanua Bi Shaibu amesema masoko makubwa ni 5 ambayo ni Buguruni,Ilala,Ferry,Kisutu na Mchikichini ambapo jumla ya wafanyabiashara wanaotumia masoko hayo ni 8,432.

Akieleza zaidi Bi Shaibu alimesema kutokana na Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Biashara ya Manispaa ya Ilala mwaka 2009,ilibainika kuwa jumla ya wafanyabishara 21,500 hawana maeneo ya kufanyia biashara na wanatumia hifadhi ya barabara na maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara.

Kutokana na hali hiyo Bi Shaibu alibainisha kuwa katika bajeti ya 2013/2014 jumla ya sh.Milioni 240 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya masoko ya Pugu ,Kigogo fresh,Kiwalani na Kinyerezi ambapo wakandarasi wameshaonyeshwa maeneo ya ujenzi kwa njia ya zabuni.

Katika hatua nyingine Bi shaibu alisema sh. Milioni 170 zimetumika kuboresha soko la Samaki feri kwa ajili ya ujenzi wa zoni ya kukaangia samaki baada ya kuungua. Pia sh. Milioni 75 zilitumika. kuboresha mifereji ya maji taka,ukarabati wa meza 23 za kunadia samaki,kuzibua mitaro ya maji taka na maji ya mvua.

Ni jukumu la wafanyabiashara wote kuzingatia usafi kwa kuhakikisha kuwa taka zinazozalishwa katika masoko yote zinahifadhiwa katika maeneo husika na kutunza mazingira ya maeneo ya masoko ili kuwalinda watumiaji wa huduma zinazotolewa katika maeneo hayo.


Friday, April 18, 2014

Fransic Miyeyusho aka CHICHI MAWE KUCHEZA MICHEZO MIWILI NDANI YA MWEZI MMOJA


Mpambano wa masumbwi wa bondia Fransic Miyeyusho na mohamed Matumla sasa utafanyika Mei 10 katika ukumbi wa PTA Sabasaba mpambano huo uliokuwa ufanyike April 26 sasa umesogezwa mbele kumpisha bondia Miyeyusho ili acheze vizuri mpambano wake wa kimataifa unao mkabili dhidi ya Bondia Sukkasem Kietyongyuth kutoka Thailand mpambano utakaofanyika April 19 katika ukumbi wa Pta sabasaba mpambano huo utakaosindikizwa na ngumi za wanawake ambapo bondia Lulu Kayake atavaana na Halima Ramadhani katika kuhakikisha mchezo wa masumbwi kwa wanawake unahamasishwa vizuri

Mshindi katika mpambano wa matumla na miyeyusho atapata nafasi ya kupata meneja kutoka katika kampuni ya Mwazoa Promosheni kutoka Tanga.

Akizungumzia maandalizi ya mpambano huo promota amesema kuwa mpambano huo utachezwa Mei 10 katika ukumbi huo wakati huohuo aliongeza kwa kusema mpambano mwingine mkali utawakutanisha mabondia Kalama Nyilawila na Thomas Mashali siku ya mei mosi mwaka huo katika ukumbi wa PTA sabasaba aliongeza kuwa katika michezo hiyo kingilio ni 7000, na 10,000 kwa viti maalumu na mchezo huo utachezwa kivyovyote iwe mvua iwe jua kwani hakuna kitu kitakachoweza kuzuia mpambano usifanyike kwa kuwa tunatumia uwanja mkubwa na uwanja wa ndani hivyo mashabiki wasisite kuja katika mechi hizo ambazo zina upinzani wa hali ya juu.


SOKA NDANI YA DSTV PEKEE



Tigo yakabidhi msaada kwa Shirika la Red Cross Tanzania kwa ajili ya waathirika wa mafuriko Dumila na Dar es Salaam

Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael (kulia) akimkambidhi mfano wa hundi cha kiasi cha Tsh 20,700,000 Kaimu Katibu Mkuu wa Shirika la Red Cross nchini Bi. Bertha Mlay jana katika hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika makao makuu ya Red Cross, jijini Dar es Salaam. Kiasi hicho kinalenga kuwapatia waathirika wa mafuriko wa Dumila - Morogoro na Dar es Salaam huduma za malazi, maji, chakula, mablanketi, neti za kuzuia mbu na magodoro.

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirika la Red Cross nchini Bi. Bertha Mlay (katikati) akipokea kwa furaha moja ya mifuko ya sembe kutoka kwa Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Tigo Bi. Halima Kasoro jana. Wafanyakazi wa Tigo waliweza pia kujichanga kiasi cha Tsh 4,000,000 ambayo imesaidia kununua vyakula hivyo.

Baadhi ya vyakula vilivyotolewa kama msaada na wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Tigo kwa waathirika wa mafuriko wa Dumila - Morogoro na jiji la Dar es Salaam jana.

Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa makabidhiano wa msaada wa fedha na vyakula kwenda kwa waathirika wa mafuriko nchini. Zaidi ya familia 800 zitanufaika na msaada huu, familia 400 kutoka Dumila - Morogoro na 400 wengine kutoka jijini Dar es Salaam. Bi. Shisael pia alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali pamoja na Shirika la Red Cross Tanzania kwa jitihada zao mpaka sasa.

Wafanyakazi wa Tigo katika picha ya pamoja nje ya jengo la Shirika la Red Cross Tanzania, jijini Dar es Salaam jana.


Tuesday, April 15, 2014

Kibonzo cha leo



Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki yazungumzia juu ya mradi wa Vituo vya Utoaji Huduma kwa Pamoja Mipakani

Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhandisi Abdillah Mataka, akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo katika kujenga vituo vya utoaji huduma mipakani kwa kila nchi husika ili kurahisisha shughuli za utoaji huduma za forodha na uhamiaji. Ujenzi wa vituo hivyo hapa nchini unafadhiliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Maendeleo ya Japan. Kushoto ni Mchumi Idara ya Biashara na Sekta za Uzalishaji kutoka wizara hiyo Bw. Amedeus Mzee. Picha na Fatma Salum.


Na Frank Mvungi.

Serikali imejipanga kukamilisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja Mipakani (One Stop Border Posts-OSBP) vitakavyosaidia kurahisisha taratibu za forodha,uhamiaji,Usimamizi wa ubora wa bidhaa na huduma ,usalama na ulinzi kwa kutoa huduma hizi upande mmoja wa mpaka.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vedastinian Jastinian wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akieleza faida za vituo hivyo, Vedastinian amesema vitaondoa urasimu uliokuwepo awali na kuharakisha huduma na kwa wananchi wa nchi wanachama wakati wanapotaka kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Alisema Kituo cha kwanza ni kile cha Holili ambacho kimekamilika na kimekabidhiwa kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao ndio waendeshaji wa vituo hivyo hapa nchini ambapo mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2014.

Alifafanua kuwa katika mipaka ya Sirari/Isebania unazitenganisha Tanzania na Kenya na kwa upande wa Mkoa wa Mara mpaka wa Mutukula unazitanganisha Tanzania na Uganda.

Vedastinian alivitaja vituo vingine kuwa ni Namanga cha Arusha,Kabanga/Kobero kilichopo mpakani mwa Tanzania na Burundi unatarajiwa kukamilika mapema mwezi novemba 2014.

Alitaja vituo vingine ni Horohoro Mkoani Tanga na Lungalunga upande wa nchi ya Kenya ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika mapema mwaka huu.

Mradi huo unatekelezwa baada ya kutungwa sheria ya jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuanzisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja mipakani (OSBP) Katika nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sheria iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na Iko katika hatua za mwisho za kuidhinishwa na Wakuu wan chi wanachama.


NGUMI KUPIGWA LEO CHALINZE MJINI


Na Mwandishi Wetu

Mchezo wa ngumi utachezwa Chalinze mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Ndelema Inn ukiwakutanisha mabondia Erick Magana kutoka Dar es salaam atakae oneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mwaite Juma leo  katika ukumbi wa Ndelema Inn Chalinze Mjini

Mpambano huo wenye upinzani mkubwa wa hali ya juu unaosubiliwa na wapenzi wa ngumi Chalinze Mkoa wa pwani pamoja na vitongoji vya jirani utakuwa chachu ya kuhamasisha mchezo uho kwa ajili ya kuibua vipaji vipya vya mchezo wa ngumi katika mkoa mzima wa pwani mbali ya mpambano huo kutakuwa na mipambano mingine ya utangulizi ambayo watapata wapinzani wao baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano huo utakaowakutanisha mabondia wa chalinze na Dar es salaam

mabondia ambao watatoka Dar kwenda kupambana na wenzao wa chalinze ni Erick Magana,Godfrey Sadiki 'Pacho Mawe',Juma Biglee,Husein Pendeza,Hamisi Kavirondo, ambao wata ongozana na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'


Mama Salma Kikwete azindua rasmi uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi huko Bahi

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Ndugu Betty Mkwasa mara baada ya kuwasili mjini Bahi kushiriki mkwenye sherehe ya uzinduzi wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi tarehe 14.4.2014.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa Macho wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Frank Magupa, wakati alipotembelea maonesho ya kitabibu yaliyofanyika sambamba na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa wilayani Bahi tarehe 14.4.2014.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Bwana Hamis Mwege kwa kazi kubwa ya kuelimisha umma kuhusu kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake hapa nchini. Vyombo vingine vilivyopata cheti ni Channel Ten na ITV. Picha na John Lukuwi.


Watumishi wa Serikali na Mashirika ya Umma wafanya Tamasha la Michezo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara ya Habara, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Barnabas Ndunguru(kushoto) na Afisa Tawala wa Wizara hiyo Bw. Mussa Varisanga wakifanya mazoezi wakati wa Tamasha la mchezo kwa ajili ya kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika mapema mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana,Utramaduni na Michezo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Michezo na Burudani kuelekea maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Bw. Leonard Thadeo wa kwanza kulia akiongoza tamasha la mazoezi ya viungo kwa Watumishi wa Serikali na Mashirika ya Umma mapema wikiendi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,Tamasha hilo ni muendelezo wa program mbalimbali za kuadhimisha Muungano kwa njia ya Mchezo na Burudani. Picha na Frank Shija.


Serikali imedhamiria kuwasaidia wajasiriamali wadogo hapa nchini

Mkurugenzi Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Tumaini Mtitu akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mikakati ya kudhibiti ubora wa bidhaa za ndani na zinazotoka nje ili kuepuka madhara kwa watumiaji wa bidhaa hizo. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa shirika hilo Bi Roida Andusamile. Picha na Fatma Salum.

Na Frank Mvungi.
Serikali imedhamiria kuwainua wajasiriamali wadogo hapa nchini ili kuongeza uzalishaji wa Bidhaa za ndani zitakazosaidia kuimarisha uchumi wa Taifa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la viwango hapa nchini (TBS) Tumaini Mtitu wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.

Alisema shirika hilo limekuwa likishirikiana na Shirika la Viwanda Vidogo (Sido) kuwajengea uwezo wajasirimali wadogo ili hatimaye wazalishe bidhaa zenye ubora na hivyo kupata cheti cha ubora kinachotolewa na shirika hilo.

Mtitu aliongeza kuwa wajasiriamali wote wanaojihusisha na uzalishaji wa bidhaa hapa nchini wanatakiwa kuthibitishwa na shirika hilo ili kuwalinda watumiaji wa bidhaa hizo kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Aliwataka Wajasiriamali hao kupitia SIDO ili waweze kujengewa uwezo wa kuzalisha bidhaa bora na baada ya hapo bidhaa zao ziweze kukaguliwa na kama zikikidhi vigezo wapate cheti cha ubora ambapo mchakato huo unaweza kuchukua mwezi mmoja.

Akizungumzia faida za Wajasiriamali kupata cheti cha ubora baada ya bidhaa zao kukidhi vigezo vilivyowekwa na shirikika hilo, Mtitu alisema unawawezesha wajasiriamali kupanua wigo wa soko la bidhaa zao na kuwa wa kimataifa.

Wakati huo huo Mtitu aliwataka watanzania wote kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali kupitia shirika hilo ili waweze kupata cheti cha ubora na kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa.

Utaratibu wa kupata alama ya ubora ni kwanza kuwasilisha maombi kwa mkurugenzi Mkuu wa TBS, ukaguzi wa awali na upimaji wa Sampuli za bidhaa husika na hatimaye kutolewa kwa cheti cha ubora baada ya bidhaa husika kukizi vigezo.


Monday, April 14, 2014

Breaking News: Ikulu yakanusha kutokuwepo kwa hati ya Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika na kuiweka wazi leo





Habari zilizotufikia hivi punde kwenye deski letu la habari inasema kwamba Ikulu imekanusha tuhuma mbali mbali zinazosema kwamba hakuna hati ya Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika kuunda Taifa la Tanzania na kuamua kuiweka wazi kwa waandishi wa habari hati hiyo asili ya Muungano huo leo hii jijini Dar es salaam. 

Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue ambae aliendelea kusema kwamba ata kama Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mh Samuel John Sitta akihitaji basi yupo tayari kuiwakilisha Bungeni hapo ili kuondoa maswali na mitazamo mbali mbali iliyowekwa mpaka sasa juhu ya swala zima la Muungano na kuzua gumzo kwa wengi.


Sunday, April 13, 2014

Azam FC Mabingwa VPL 2013/2014


Azam FC wamefanikiwa kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.


Liverpool yaifunga Man City 3-2 kuendelea kujitengenezea nafasi ya kubeba Ubingwa ligi kuu ya England


Mchezaji wa Liverpool Philippe Coutinho akifunga bao la ushindi kwa timu yake baada ya Vincent Kompany kufanya makosa (kupiga fyongo) yaliyosababishia mpira kufika kwa Coutinho na kufunga goli la ushindi


Breaking News: Helkopta iliyombeba Makamu wa rais yapata ajari



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa polisi Kanda Maalum, Suleman kova pamoja na Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli wamenusurika kufa katika ajali ya Helkopta wakati wakiwa wakitaka kuruka kwenda kwenye ukaguzi wa uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua kubwa jijini Dar es salaam. Hakuna aliyepoteza maisha wala kuumia.


Breaking News: muhidin maalim gurumo afariki dunia


Habari zilizotufikia hivi punde zinasema, mwanamuziki muimbaji wa siku nyingi Mzee Muhidin Maalim Gurumo hatunae tena.

Mzee Gurumo amefariki alasiri hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Mungu ailaze roho yake mahali Pema Peponi..Amin


JK akagua barabara zilizoaribiwa na mvua zinazoendelea kunyesha mlandizi bondeni, mkoa wa pwani




Picha zote na Josephat Mrema wa Changanua Blog.


Arsenal overcome Wigan in penalty kicks to advance to FA Cup final


Arsenal's goalkeeper Lukasz Fabianski Saved two penalties in Arsenal's shootout success


Saturday, April 12, 2014

Matukio ya Bunge la Katiba katika Picha leo

Wajumbe wa Bunge Maalum la KatibaTundu Lissu(kushoto) akisalimiana na Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) mara baada ya kikao cha Bunge hilo leo mjini Dodoma. Kulia ni Mchungaji Peter Msigwa

Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiondoka katika eneo la Bunge leo mjini Dodoma baada ya kikao kuharishwa. Picha na Bunge Maalum la Katiba.


Mafunzo ya wiki mbili kuhusu Uongozi katika Mkakati wa Mawasiliano ya Afya yamalizika mjini Iringa

Washiriki wa mafunzo ya wiki mbili kuhusu Uongozi katika Mkakati wa Mawasiliano ya Afya, yanayofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia mradi wa Tanzania Capacity and Communication Project (TCCP),wakiwa katika picha ya pamoja mara baada kuhitimu mafunzo hayo yaliyomalizika leo hapa mjini Iringa. Picha na Immaculate Makilika


Kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha hayati Edward Moringe Sokoine Wilayani Monduli

pika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili kushiriki misa ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowasa, wakishiriki Misa maalum ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.


Mhe. Rais akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.

Mhe. Lowasa nae akiweka shada.


Waziri Mkuu akutana na Timu Bingwa wa Dunia ya watoto wa mitaani

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na mabingwa wa Dunia wa kombe la duniani kwa watoto wa mitaani mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Juma Nkamia ( wa pili kulia) akitoa utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuongea na mabingwa wa Dunia wa kombe la duniani kwa watoto wa mitaani mjini Dodoma, kushoto ni Rais wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) Altaf Hirani.

Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda akipiga picha na mjukuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi katikati ni Rais wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) Altaf Hirani mjini Dodoma huku wakiwa na Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani wa Tanzania walilolipata nchini Brazil.


Kampuni ya Jubilee yamkabidhi Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda kadi Maalum ya Bima ya Afya

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Ndg. George Alande (kushoto), Ndg. Peter Nyabuti kutoka kampuni ya ushauri wa Bima ya Astra Insurance Brokers (Kulia) na Bi. Kitolina Kippa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Bunge.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Ndg. George Alande akimkabidhi Mhe. William Lukuvu kadi Maalum ya Bima ya Afya atakayoitumia kwa ajili ya matibabu baada ya Ofisi ya Bunge kujiunga na kampuni ya Jubilee Insuarnce kwa ajili ya Bima ya matibabu ya Wabunge wote. Anaeshuhudia katikati ni Ndg. Peter Nyabuti kutoka kambuni ya ushauri wa Bima ya Astra Insurance Brokers. Picha na Owen Mwandumbya.


Friday, April 11, 2014

MABONDIA MIYEYUSHO,CHEKA,KING CLASS MAWE WAPIMA UZITO KUPAMBANA JUMAMOSI APRIL 12 PTA SABASABA

Bondia Sukkasem Kietyongyuth kutoka Thailand akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa jumamosi ya April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.

Bondia Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba kushoto ni bondia Gavad Zohrehvand wa Iran

Bondia Mustafa Dotto kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'KIng class Mawe' kabla ya kuzipiga katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi katikati ni Promota Jay Msangi Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com