Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akimkabidhi kijarida cha Mfuko huo chenye maelezo ya shunguli mbalimbali zinazotekelezwa na PSPF, kwa Mwanachama wa Mfuko amabye ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mstaafu, Mzee Thomas Martin Kiama, (73), nyumabni kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja leo Oktoba 6, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto, ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, na Afisa wa Unedeshaji Bw. Ernest Massay.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambao ni wastaafu, wameupongeza Mfuko huo kwa kupata pensheni za kila mwezi kwa wakati.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya viongozi wa PSPF kutembelea Wanachama wake wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, walisema kimsingi malipo ya pensheni ya kila mwezi yamekuwa yakiingia kwenye akaunti zao kwa wakati na bila usumbufu wowote.
“Mimi nashukuru penshni yangu napata bila shida, na inaingia kwenye akaunti yangu kwa wakati, hili napenda kuwapongeza sana.” Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu). Bw. Thomas Martin Kiama wakati alipotembelewa na ujumbe wa PSPF nyumbani kwake Oysterbay jana (Oktoba 6, 2017).
Najua zipo changamoto za hapa na pale, mimi ningependa muwe huru kabisa, ili muweze kutuhudumia vema sisi wanachama, vinginevyo huduma zenu nazifurahia, aliongeza Bw.Kiama, ambaye alistaafu mwaka 2005.
Kwa upende wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, nchini, Bibi. Mary Hariet Longway, naye aliipongeza PSPF kwa utoaji wa huduma na kwamba yeye anaridhishwa na utedaji kazi wake na kuwapongeza kwa kufika nyumbani kwake ili kupata maoni yake.
“Ninashukuru sana kwa kunitembelea kwani hii ni ishara ya jinsi mnavyotujali sisi wastaafu, lakini mimi kama Jaji mstaafu kwa utaratibu ulivyokuwa, sisi hatukuwa na bima za afya sasa kama mngetoa elimu ya jinsi ya kupata bima ya afya kupitia kwenu lingekuwa jambo jema.” Alishauri Bibi Longway amabye naye alistaafu mwaka 2005.
Alsiema, malipo ya kila mwezi ya Pensheni yake yamekuwa yakiingia kwenye akaunti yake bila shida yoyote.
Naye askari wa Jeshi la Magereza (mstaafu), Bw.Kasim Salehe Mafanya, yeye naye aliipongeza PSPF, kwa huduma bora lakini akaomba utaratibu ufanyike ili pensheni hiyo iweze kuboreshwa na hivyo kuelndelea kuwa na manufaa zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya PSPF, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Bi. Mwanjaa Sembe, alisema, katika kuadhimisha Wiki ya Wateja Duniani, ofisi za PSPF kote nchini, zimefanya utaratibu wa kuwatembelea wanachama wake kwa lengo la kuwahakiki na kupokea maoni yao ili kuboresha utoaji wa huduma.
Aidha katika Ofisi za Makao Makuu, Wakurugenzi an Mameneja waliungana na maafusa na wafanyakazi wa Mfuko huo, katka kuwahudumia wateja waliofika makao makuu.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Bibi Mary Logway, ambaye ni mwanachama wa PSPF, akizungumza nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam leo Oktoba 6, 2017, wakati alipotembelewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, kushoto.
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wakwanza kushoto), akimsikilzia mteja (mwanachama) wa Mfuko, huku afisa aliye kwenye mafunzo kutoka Chuo Cha Usimamzi wa Fedha, (IFM), Bw. Paschal W. Divaz, (katikati), akifuatilia.
Bw. Silayo akisalimiana na wateja (wanachama) waliofika makao makuu ya Mfuko kuhudumiwa.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro, (kulia), akimuhudumia mteja (mwanachama) aliyekifa makao Makuu kuhudumiwa.
Meneja wa Huduma kwa Wateja, PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na mteja wake, (mwanachama) wakifurahia jambo wakati mwanachama huyo akipatiwa huduma. |
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, wapili kulia), akizungumza na afisa aliye mafunzoni, kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha, 9IFM), Bw.Paschal W. Diaz
Afisa Uchangiaji wa Hiari PSS, Bi.Mwajuma A.Mohammed, (kushoto), akimuhudumia mteja.
Afsia Mtekelezo, (CO), wa PSPF, Bi. Mwanaisha S. Waziri akiwa kazini.
Afisa wa PSPF aliye mafunzoni, Bw. Alpha Mkopi, (katikati), akiwahudumia wateja, waliofika ofisi za Makao Makuu kupata huduma.
Maafisa wa PSPF wakitoa huduma Oktoba 6, 2017. |
Mzee Kiama, (kushoto), akipitia maelezo ya uhakiki kabla ya kuweka saini yake. aliye nae ni Meneja wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe. |
Mzee Kiama akiweka saini kwenye fomu ya uhakiki.
Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimpa maelezo, Jaji Mstaafu, Bi. Mary Longway, kuhusu uhakiki wa uanachama wake PSPF. |
Bi. Longway akiweka saini wkenye fomu hiyo ya uhakiki. |
Mkuu wa kitengo cha Mikopo kwa Wanachama wa PSPF, Bi. Linda Bahati, akizungumza na simu ya kikazi ili kupata maeelzo ya ziada wakati akimuhudumia mteja Oktoba 6, 2017.
Afisa Uhsuiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akizungumza na Mzee Kiama.
Jaji (mstaafu) Longway na mukuu wake, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyaakzi wa PSPF waliomtembelea ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment