Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, December 25, 2017

UBALOZI WA KUWAIT WAKABIDHI VIFAA VYA WALEMAVU MKOANI TABORA

Kutoka kushoto, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mh. Jasem Al-Najem, Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Stella Ikupa, na Mwenyekiti wa Dr Amon Mkoga Foundation. Ubalozi wa Kuwait umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora.


Friday, December 22, 2017

SALAMU ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA PSPF



Monday, December 18, 2017

WATANZANIA WAASWA KUPENDA BIDHAA ZA NDANI

Watanzania wameshauriwa kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa nchini ili waweze kukuza soko la ndani na uchumi kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Meneja Masoko, Tafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA (BOA), Muganyizi Bisheko, wakati alipokua akikabidhi msaada wa vyerehani kwa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Alisema ili uchumi wa nchi wanchi ukue haraka, watanzania wanapaswa kubadili mitazamo ya kudhani kuwa bidhaa za nje ni bora kuliko bidhaa za ndani, jambo ambalo si sahihi.

Alisema katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia, Watanzania wengi wamepiga hatua katika uboreshaji wa shughuli zao, jambo ambalo limechangia kuwepo kwa bidhaa bora zinakubalika katika soko la ndani nan je ya nchi.

“ ifike wakati Watanzania tunapaswa kubadili mitazamo yetu na kuamini kuwa, bidhaa zinazozalishwa nchini zina ubora unaokubalika, jambo ambalo linachangia kupata masoko ya ndani na njke ya nchi”, alisema Bisheko.

  Alisema Benki hiyo inashirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo wamiliki wa vyuo na viwanda vidogo ili kuhakikisha wanaboresha shughuli zao na kujiongezea kipato.

Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Oystebay, Sister Getrude Amandus, alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ya ufundi ili kuwawezesha vijana kujiajiri.

Meneja Masoko, Tafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA (BOA), Muganyizi Bisheko, akikabidhi msaada wa vyerehani kwa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi kilichnopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Monday, December 11, 2017

NJIA SALAMA ZAIDI YA KUTUMIA INTANETI MAJUMBANI NA MAKAZINI

Baada ya Smile Communications Tanzania kupunguza bei na kuongeza thamani kwenye vifurushi vyake vya internet, wateja na wapenzi wa 4G nchini Tanzania wamekuwa wakifurahia intaneti yenye kasi na muda zaidi, kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kimewashawishi wafanyabiashara na wananchi, hasa wazazi na wamiliki wa nyumba wenye bajeti ndogo kutumia mtandao huo.

Ingawa matumizi ya intaneti yamerahisishwa sana, hasa kupitia teknolojia ya 4G, bado kumekua na uhitaji mkubwa wa usalama pindi wateja wanapokuwa mitandaoni. Wateja wengi hasa wafanyabiashara na wazazi wamekua wakijiuliza ni kwa jinsi gani watoto na waajiriwa wao wataweza kutumia intaneti kwa manufaa na si vinginevyo. Kutokana na wasiwasi huo Smile Tanzania ikawaletea watanzania uwezo wa kudhibiti matumizi ya vifaa vyao hata kupitia kwa simu zao za mkononi, suluhisho ambalo limepokelewa vyema sana na wapenzi wa mtandao wa 4G nchin Tanzania, hasa wale wanaojali usalama wa watoto wao na wafanyakazi wao pindi wawapo mtandaoni.

Wateja wa Smile sasa wanaweza kutumia akaunti zao za "MySmile" kudhibiti matumizi ya vifaa vyao kadri wanavyopenda, ikiwapa nguvu za kufanya mengi kupitia vipengele vilivyoongezwa. Baadhi ya vipengele vilivyopatikana kwenye MySmile Portal ni kama ilivyoorodheshwa hapa chini.

Historia na Grafu ya Matumizi: Hii inaruhusu mtumiaji kufuatilia matumizi yake ya kila siku na shughuli zilizofanywa kutoka kwa akaunti yake ya MySmile

Uwezo wa kudhibiti line na vifaa zaidi ya kimoja kwa Akaunti moja tu: Kipengele hiki kinawawezesha wateja wa Smile kuwa na udhibiti wa vifaa vyao vyote kwa kutumia akaunti moja tu

Nguvu ya kudhibiti matumizi ya vifurushi kwa kudhibiti vipengele: Baadhi ya vipengele ni downloads za automatic – unazoweza kuzizuia kwa kuingia tu na kuchagua "Manage my data usage ".

Mteja wa Smile anaweza pia kuzuia Uhifadhi wa Cloud, Torrent na Video kupitia MySmile kitu kitakachompa matumizi rahisi zaidi ya vifurushi, hususan unaposhea mtandao (wireless) na watumiaji wengi kwa kuunganisha na vifaa vyao kupitia Wi-Fi kwenye Router moja au MiFi.

Kupitia MySmile Pia mteja anaweza kudhibiti kasi ya vifurushi vyake wakati wote: Ni kweli! Ingawa Smile inakupa kasi kubwa Zaidi ya 4G nchini Tanzania, mteja ana chaguo la kutumia kikamilifu au kuipunguza kasi ya mtandao kadri apendavyo. UKIWA NA SMILE PEKEE!

Kuna faida nyingi ambazo wapenzi wa mtandao wa 4G na wateja wa Smile wanaweza kufurahia kila siku kupitia vifurushi vya Smile 4G. Zaidi ya hayo, Smile pia hupendekeza njia rahisi ambazo zinaweza kusaidia wateja wao kuona jinsi vifurushi vyao vinatumiwa. Mawakala wa Smile Huduma kwa wateja wako tayari kutoa ushauri juu ya jinsi ya kuepuka matumizi yoyote yasiyotakiwa. Tafadhali wasiliana na 0662 100 100 kwa maelezo zaidi au, kwa njia ya barua pepe customercare@smile.co.tz


Saturday, December 9, 2017

SALAMU ZA MIAKA 56 YA UHURU KUTOKA PSPF



Thursday, December 7, 2017

UTT AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA WANANCHI MBALIMBALI NA WASHIRIKI WA SEMINA JIJINI MOROGORO

Maafisa wa UTT AMIS wakitoa elimu ya jinsi mifuko ya Uwekezaji wa pamoja inayosimamiwa na kampuni hiyo na kwamba ni suluhisho kubwa la maisha baada ya kustafu katika semina iliyoandaliwa na National Institute of Productivity (NIP) jijini Morogoro.