Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, July 17, 2017

BANK OF AFRICA YAKABIDHI RASMI MTAMBO WA UJENZI AINA YA GREDA KWA MTEJA WAKE

Naibu Mkurugenzi mtendaji wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Wasia Mushi akikabidhi mfano wa funguo kuashiria makabidhiano ya Greda kwa Mteja Bw. T Hitesh Vishram ambae ni Project Supervisor wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Limited, Katikati ni meneja wa masoko, Utafiti na maendeleo wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Muganyizi Bisheko.


BANK OF AFRICA hii leo imekabidhi rasmi mtambo wa ujenzi (Greda jipya aina ya JCB) lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300 kwa kampuni ya Dezo Civil Contactors Limited, kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo kandarasi ya ujenzi wa kuta kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi.

Makabidhiano ya mtambo huu ni sehemu ya mpango endelevu wa benki wa kununua na kukodisha mitambo (lease finance), ambayo inawawezesha wateja kujiongeza kiutendaji kwa kupata vifaa vya kisasa bila ya kulazimika kuwa na pesa taslimu za manunuzi ya vifaa hivyo.

Makubaliano haya ya ukodishaji wa mitambo yanaakisi katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano, utalii, madini, mafuta na gesi.

BANK OF AFRICA imebaini huu ni mpango ambao una tija kubwa kwa wajasiriamali wakubwa kwa wadogo, kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa biashara zao ambao utaongeza uzalishaji na faida kubwa. Mteja kupitia mpango huu anapewa fursa pana ya kufanya chaguo lake bila kikwazo chochote na bila ya uhitaji wa amana ya awali au dhamana nyingine. Marejesho ni malipo ya ukodishaji ya kila mwezi na mteja ana uwezo wa kuchagua kua mmiliki wa mali husika pindi ifikapo mwisho wa mkataba wa ukodishaji.

Benki humsaidia mteja kuhakiki chombo anachotaka kuingianacho mkataba kama kina ubora ili kuweza kuinua uchumi wake na uchumi wataifa kwa ujumla.

BANK OF AFRICA ilianza shughuli zake Juni mwaka 2007, baada ya kuinunua Benki ya Euroafrican ambayo ilianza kazi Tanzania kutokea September 1995.

BANK OF AFRICA inafanya kazi katika mtandao wa benki za biashara katika nchi 18 zikiwamo nchi za Benin, Burkina Faso, Burundi, Cote d”ivoire, Djibouti, DRC, Ethiopia, France, Ghana, Kenya, Madagascar, Mali, Niger, Rwanda, Senegal, Tanzania, Togo na Uganda.

Kundi la Group BANK OF AFRICA lina makao makuu yake jijini Dakar, Senegal ikiwa na mtandao wa watu 500 wale wanaotoa huduma na sapoti kwa ofisi. Kuanzia mwaka 2010, Group BANK OF AFRICA ilimilikiwa kwa wingi wa hisa BMCE Bank, ambayo ni benki ya pili kwa ukubwa nchini Morocco.

BMCE Bank huleta mikakati mizito ya msaada wa uendeshaji katika kuunga mkono shughuli za BANK OF AFRICA Group, vilevile na muunganiko na ukaribu wa kufikia masoko ya kimataifa kutokana na uwepo wake katika nchi za Ulaya na Asia.


BRAZUKA KIBENKI: Maofisa kuonyeshana kazi viwanjani

MSIMU wa tatu wa michuano ya BRAZUKA KIBENKI unaoshirikisha taasisi za kibenki katika michezo ya mpira wa miguu na kikapu unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.
Katika msimu huu michuano hiyo itashirikisha timu 15 ambazo ni NMB (Mabingwa watetezi), DTB, Barclay’s, BancABC, Exim, Stanbic, BOA, UBA, Letshego, EcoBank, CRDB, BOT, Azania, TPB, Access na UBA.
Mmoja wa maofisa wa benki ya Exim, Frank Rweyemamu ambaye pia ni mwanachama wa tawi la Simba Makini linalomiliki mtandao huu alivitaja viwanja vitakavyotumika kuwa ni Gymkhana na DonBosco.


Martin Komba wa DTB (kulia) akimtoka
Hezbo wa NMB katika pambano la jana

“Michuano ya mwaka huu itafanyika katika viwanja vya Gymkhana kwa mpira wa miguu huku mechi za mpira wa kikapu zikitarajiwa kuchezwa katika uwanja wa DonBosco.” Alisema Rweyemamu.
Jana kulikuwa na mchezo wa ngao ya hisani ambapo mabingwa watetezi NMB walikubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa DTB katika mchezo wa kuashiria kuanza kwa michuano hiyo.
Bingwa wa msimu huu atakabidhiwa kikombe pamoja na medali.


Saturday, July 15, 2017

SEMINA YA PSPF KWA WASTAAFU WATARAJIWA: NAIBU WAZIRI JAFO AHIMIZA WAAJIRI KUWASILISHA MICHANGO YA WANACHAMA KWA WAKATI



Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akikabidhiwa fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Mfkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, (kulia), baada ya kufungua semina ya Mafunzo kwa wastaafu watarajiwa mkoni Dodoma Julai 14, 2017.


NA K-VIS BLOG, DODOMA
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani Jafo amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS) na kuhimiza na kjtoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati kama sheria inavyowataka ili kuepuka usumbufu kwa wanachama wakati wa kupata Mafao yao wanapostaafu. 
Mhe. Jafo aliyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa  mkoani Dodoma Julai 14, 2017.
Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wastaafu hao watajiwa ili kuweza kufanya shughuli za ujasiriamali wakati muda wao wa utumishi wa umma utakapokoma.
Mhe. Jafo amewanyooshe kidole waajiri wenye tabia ya kutopeleka michango ya wanachama katika mifuko yao kitendo ambacho kinasababisha kero kubwa pindi watumishi hao wanapostaafu na kuanza kuhangaikia Mafao yao kutokana na taarifa za uwasilishaji michango katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutokamilika.

“Nitoe rai kwa ndugu zangu watumishi wa umma ambao katika kipindi cha miaka miwili ijayo mtaondoka kwenye utumishi wa umma, yatumieni vema mafunzo haya ili mtakapopata mafao yenu basi tayari mtakuwa na nyenzo ya kuwasaidia kutumia vema fedha mtakazopata kwa kuanzisha  viwanda vidogo vidogo, lakini pia kilimo na ufugaji wa kisasa na hatimaye kuyafanya maisha yenu kuwa bora baada ya utumishi wa umma.” Aiasa Mhe. Jafo.
Katika hatua nyingine, wimbi la viongozi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari yaani PSPF Supplementary Scheme, (PSS), Mhe. Jafo naye amejiunga na mpango huo na kuwahamasisha wastaafu hao watarajiwa na wananchi wengine kujiunga na Mpango huo kwani utawawezesha kuwa na hakikisho la kuweka fedha zao ili ziwasaidie kwenye miradi wanayotarajia kuibuni, ikiwa ni pamoja na kujipatia bima ya afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu, amebainisha kuwa mfuko huo unatarajia kulipa jumla ya Sh.Trilioni 1.3 katika kipindi cha 2017/18 ambazo ni Mafao ya watumishi 9,552 wanaojiandaa kustaafu katika kipindi cha kati ya Mwaka huu wa 2017 na mwaka ujao wa 2018.

 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akitoa hotuba yake. "Mfuko umetenga kiasi cha shilingui Bilioni 1.3 kwa ajili ya kulipa mafao watumishi 9,552 wanaotarajiwa kustaafu kati ya mwaka huu wa 2017/2018."
 Naibu Waziri Jafo akitoa hotuba yake.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.


Mzee mstaafu akitoa ushuhuda kwa kundi la wanachama wa Mfuko wa PSPF wanaotarajiwa kustaafu katika semina iliyoandaliwa na mfuko huo mkoani Dodoma.


Saturday, July 8, 2017

MAONESHO YA SABASABA 2017:WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA KUHIMIZA WANANCHI KUFANYA HIVYO ILI KUFAIDIKA NA BIMA YA AFYA


 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kulia), akikabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, muda mfupi baada ya Mhe. Waziri kujiunga na Mpango huo leo Julai 8, 2017, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ambapo PSPF inatoa huduma zote kwenye Maonesho hayo.
Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akimsikilzia kwa makini Bw. Njaidi kuhusu faida zitokanazo na kujiunga na Mpango wa PSS
 Waziri Dkt. Mpango(kulia), akipokea fomu ya kujiunga na PSS, kutoka wka Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii maarufu, Mrisho Mpoto. Katikati ni Afisa Habari Mwanamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Habari na Picha wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Rodney Thadeus, akiweka dole gumba kwenye fomu ya kujiunga na uanachama wa PSPF kupitia PSS, leo Julai 8, 2017


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,(pichani) amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo kwani moja ya faida kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya Afya.
Waziri aliyasema hayo leo Julai 8, 2017, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasabawakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea.
“Mimi nitoe wito kwa wananchi kujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi.” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango pia alikabidhiwa kadi yake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.
“Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, na machinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo mwananchama” Alisema Afisa Uhusoano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.

Bw. Njaidi pia alimwambia Mhe. Waziri kuwa, kwa kujiunga kwake na Mpango huo wa uchangiaji wa Hiari, kutasaidia pia kuwakadia bima ya afya wasaidizi wake katika miradi kama vile ya shambani na ufugaji.
“ Hawa wote wanawezakuingia kwenye mpango huu wa bima kupitia uanachama wako katika Mfuko.” Alimuhakikishia Mhe. Waziri.

 Waziri Mpango (kulia), akiuliza maswali kwa maafisa wa PSPF
 Mwananchi akisoma kipeperushi chenye taarifa za PSPF alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
 Baada ya Mwanachi huyu kuelewa huduma za PSPF na faida zake kwake, hatimaye alikata shauri la kujiunga na Mpango wa PSS, kwa kujaza fomu kama picha hii inavyojieleza.
 Waziri Dkt. Philip Mpango, (kulia), akipokea mkoba wenye vipeperushi vya taarifa mbalimbali za PSPF, kutoka kwa balozi wa Mfuko huo, Msanii maarufu Mrisho Mpoto baada ya kutembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
 Mhandisi Ally Shanjirwa wa PSPF, akiwapatia maelezo wananchi hawa waliofika kutembelea banda la Mfuko huo
 Bw.Noah Amri, (kulia), Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akizungumza na mwanchi huyu aliyeshika fomu yakujiunga na Mpango huo
Maafisa wa PSPF wakiwa kazini.


Saturday, July 1, 2017

RC KILIMANJARO, MHE. ANNA NGWIRA, AIPONGEZA PSPF KWA KUENDESHA MAFUNZO KWA WASTAAFU WATARAJIWA


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, (kulia), akipokea kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kupitia mpango wa hiari, (PSS), kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, wakati wa semina ya wastaafu watarajiwa mkoani Kilimanjaro Juni 30, 2017.

 Bw. Mayingu akitoa hotuba yake
 Mhe. Anna Ngwira, Mkuu wa Mkaow a Kilimanjaro, akionyesha kadi yake ya uanachama wa PSPF kupitia mpango wa PSS

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira,akiagana na wanachama wasitaafu watarajiwa,wa mfuko wa pesheni wa PSPF,mara baada ya kufungua semina hiyo Mkoa wa Kilimanjaro Juni 30, 2017

Baadhi ya wastaafu watarajiwa wakiwa kwenye semina ya mafunzo iliyoandaliwa na PSPF mkoani Kilimanjaro
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPF
 Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo
Baadhi ya wastaafu watarajiwa wakiwa kwenye semina ya mafunzo iliyoandaliwa na PSPF mkoani Kilimanjaro