Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, May 30, 2016

Klabu ya Rotary ya Oyster Bay Yatoa Huduma za Afya kwa Wanafunzi zaidi ya 950 wa Shule Mbili za Msasani

Dakitari wa macho akiwa katika jukumu la kumpima macho mwanafunzi wa shule ya msingi msasani

Rais wa klabu ya Rotary ya Oyster bay jijini Dar es Salaam, Bwana Mohammed Versi akizungumza na wanahabari

Baadhi ya madakitari wakiwa katika majukumu yao ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata matibabu

Dar es Salaam, 29 Mei 2016
Klabu ya Rotary ya Oyster Bay ya jijini Dar es Salaam imeandaa kambi ya matibabu na kutoa huduma za afya kwa wanafunzi wa shule mbili za Msasani, Msasani A na Msasani B na kufanikiwa kutoa huduma kwa wanafunzi zaidi ya 950. Kambi hiyo ya siku moja ilitoa vipimo vya afya, ushauri, matibabu na huduma mbalimbali za meno, macho, malaria, usafi wa mwili, minyoo, masikio, pua na koo (ENT), pamoja na magonjwa ya ngozi. Kampeni ya Damu Salama pia ilifanyika wakati wa kambi hiyo ili kuwawezesha uchangiaji wa damu katika benki ya damu salama.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa klabu ya Rotary ya Oyster bay jijini Dar es Salaam, Bwana Mohamed Versi alisema waliguswa kufadhili upimaji huo kwa sababu suala la afya ni jambo la msingi kwa mwanadamu
"Rotary tumekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii, na hii si mara ya kwanza kusaidia shule hii, tayari tumeshajenga maktaba mbili, tumeweka maji safi na salama, tumepanda miti, tumejenga ukuta ili kuimarisha ulinzi na awamu hii tumeona ni vyema tutoe huduma ya afya"

Uongozi wa shule ya msingi Msasani umesema umefurahishwa na kitendo cha klabu ya Rotary ya Oyster Bay kwa kutambua kuwa afya njema ni silaha bora kwa mtoto katika mafaniko ya kielimu.
"Nawashukuru mno Rotary maana wamekuwa washirika waaminifu wa vitendo na si maneno pekee.

Bado tunaomba wadau wengine waige mfano huu katika kutusaidia, bado tuna changamoto mbalimbali zinazotukabili" alisema mwalimu mkuu wa shule hiyo, Egidius Mjumangoma
Kambi hiyo ya matibabu ni muendelezo wa huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa na klabu hiyo katika shule za Msasani A na B. Miradi katika shule hiyo ilianza katika eneo la maji na usafi ambapo shule hizo zilipatiwa maji safi na salama ya kunywa pamoja na ya matumizi mengine.

Klabu hiyo pia ilifanya ukarabati wa majengo na kuweka vitabu katika maktaba mbili kwenye shule hizo. Maktaba hizo zina vitabu vipya na vinavyovutia kwa matumizi ya watoto, makabati yenye vitabu vipya vipatavyo elfu nne (4,000) vingi vikiwa katika lugha ya Kiswahili, ili kutoa hamasa ya kusoma kwa watoto wadogo.

Klabu hiyo ya Rotary Oyster Bay, kwa sasa iko katika ujenzi wa ukuta kuzunguka shule hizo ili kuweka usalama wa mali za shule pamoja na wanafunzi. Ujenzi huo umewezeshwa na fedha zilizopatikana kutoka kwenye mojawapo ya shughuli za ukusanyaji fedha zinazofanywa na klabu hiyo. Mojawapo ya kazi zilizofanyika wakati wa kambi ya matibabu ilikuwa ni ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukuta huo ambapo wanaklabu na wageni waalikwa walishiriki katika ziara hiyo.

Kambi hiyo ya matibabu imefanyika kwa udhamini wa Diamond Trust Bank, Whitedent, Knight Support, Vital Supplies, Mansoor Daya, Cello na Sayona kwa ushirikiano na Hindu Mandal Hospital, TDA, Damu Salama na wanafunzi kutoka Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) na Hubert Kairuki Memorial University (HKMU).

Maktaba hizi mbili zilifadhiliwa chini ya mpango uitwao “Rotary Global Grant”, ambapo katika tafsiri za Rotary, ni pale ambapo Rotary International na ofisi ya Rotary katika kanda husika hutoa msaada wa kifedha kwa klabu yoyote ya Rotary ndani ya kanda. Klabu inayopewa ufadhili huo inatakiwa kushirikiana na klabu yoyote kutoka kanda nyingine ili kuendesha mradi wa jamii ulio endelevu na ambao matokeo yake yanaweza kupimika.

Baada ya shule hizo kuchukuliwa chini ya uangalizi wa Klabu ya Rotary ya Oyster Bay, miradi mingine inapangwa kufanyika katika shule hizo mbili ambapo mafunzo kwa walimu yameandaliwa kufanyika ndani ya mwaka huu. Walimu wa shule hizo watapewa mafunzo ya namna ya kufundisha watoto, yani namna na kutumia maktaba hizo mpya kwa lengo la kukuza kiwango cha uelewa kwa watoto wadogo kwenye jamii zetu.


Saturday, May 28, 2016

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MZEE MAKWAIA



likuwa siku, miezi na leo hii ni mwaka wa tatu tangu ulipotuacha kwa machungu mengi siku ile ya tarehe 30th May 2013 ukiwa Jaslok Hospital, India. Kimwili haupo nasi bali kiroho tupo nawe, Daima tunamshukuru Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi, Sio tu kuwa Baba mwenye upendo bali kwa kuwa ulikuwa mtu wa pekee miongoni mwetu. Uliyebarikiwa kwa mambo mengi, ucheshi wako, hekima na busara zako, na juu ya yote hayo ulikuwa unafanya jambo kwa kusudi maalumu kwa kupenda usawa kwa kila binadamu, na kuwataka watoto wako tuwe na upendo na kutambua umuhimu wa elimu katika familia na jamii.

Tutaendelea kukumbuka na kufuata ushauri wako na mema mengi uliyotufundisha, na daima tutaendelea kukumbuka busara zako Baba na tutaendelea kukuenzi hadi tutakapo kutana tena paradiso.


Daima unakumbukwa sana na mke wako Mama Thecla Makwaia; watoto wako Stella Makwaia, Frank Makwaia, Robert Makwaia na Christopher Makwaia (MK), wajukuu zako Magdalen Christopher Makwaia pamoja na Madeleine Christopher Makwaia, unakumbukwa sana na ndungu zako, marafiki zako, majirani zako wote, wafanyakazi wenzako na Idara mbali mbali ulizowahi kufanyakazi kipindi cha uhai wako.


Tutakukumbuka daima Baba.


PUMZIKA KWA AMANI. AMEN.


*Misa ya kumbukumbu itafanyika tar 29/05/2016 saa 2.30 asubuhi katika kanisa la Maximilian Kolbe – Mwenge Afrika Sana.


Sunday, May 22, 2016

TIBA ASILIA YA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA WANAUME



Je wewe ni mwanaume unayesumbuliwa na tatizo la ukosefu & upungufu wa nguivu za kiume lililo sababishwa na athari za kujichua kwa muda mrefu?

Unahitaji tiba ya uhakika ya tatizo lako ? Kama jibu ni NDIO basi hii ni HABARI NJEMA SANA KWAKO.

NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC ni duka linalo uza dawa mbalimbali za asili.

Tunayo dawa asilia iitwayo JIKO ambayo inatibu na kuponyesha kabisa tatizo la ukosefu na upungufu wa nguvu za kiume ndani ya siku thelathini.

Dawa hii ni ya asilia kabisa (Pure Herbal ) ambayo haijachanganywa na kemikali yoyote ya viwandani na IMETHIBITISHWA NA MKEMIA MKUU WA SERIKALI.

Dawa hii inapatikana kwa gharama ya SHILINGI ELFU THEMANINI ( Tshs.80,000/=) TU ZA KITANZANIA.

Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA.

Kwa wateja waliopo jijini Dar Es Salaam, wasio weza kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ), kwa wateja wa mikoani na nchi jirani watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi, kwa wateja waliopo Zanzibar watatumiwa dawa kwa njia ya boti na kwa wateja waliopo ughaibuni watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.

Kwa mahitaji ya dawa ya JIKO, wasiliana nasi kwa simu namba 0766 53 83 84.

Kufahamu jinsi suala la kujichua linavyo sababisha tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume na jinsi dawa ya Jiko inavyo fanya kazi ya kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, tembelea; http://www.neemaherbalist.com/2015/07/ijue-sayansi-ya-mfumo-wa-nguvu-za-kiume.html