Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Changanua Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Tuesday, August 4, 2015

Mh Anne Makinda ashiriki Maadhimisho ya siku ya Mwanamke wa Afrika yaliyo ratibiwa na WiLDAF jijini Dar es salaam

Maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 31 July toka tamko rasmi la Umoja wa Afrika mnamo mwaka 1962 lililotolewa jijini Dar es Salaam -Tanzania.

WiLDAF Tanzania imekuwa ikiratibu maadhimisho haya hapa nchini ikiwa pia ni siku maalumu ya kusherehekea mafanikio ya wanawake wa Afrika. Katika maadhimisho hayo WiLDAF ilizindua ripoti ya kwanza ya hali za haki za Wanawake nchini Tanzania ya mwaka 2014 iliyozinduliwa na Mh. Anne Makinda, (SPIKA wa Bunge).

Maadhimisho haya yalifanyika siku ya ijumaa tarehe 31 July 2015 katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Mh. Anne makinda akiwasili ukumbini pamoja na mwenyekiti Mh Naomi Kaihula na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya WiLDAF Edda Mariki, na mkurugenzi ‎mtendanji wa WiLDAF Dkt Judith Odunga .

Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt. Judith Odunga akimshukuru Mgeni rasmi Mh. Anne Makinda katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika.

Mgeni rasmi Mh. Anne Makinda akizindua ripoti ya hali za hali za wanawake nchini Tanzania ya mwaka 2014 iliyoandaliwa na WiLDAF

Mgeni rasmi Mh Anne Makinda akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Wanawake wa Afrika iliyoandaliwa na WiLDAF

Washiriki kutoka mashirika mbalimbali wakifuatilia mada katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa afrika iliyoandaliwa na WiLDAF

Mama Laeticia Mkurasi akihamasisha wanawake kutitokeza katika uchanguzi mkuu, katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika yaliyoandaliwa na WiLDAF

Mwadhiri kutoka katika chuo kikuu cha Bagamoyo Natujwa Mvungi, akichangia mada katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa afrika yaliyoandaliwa na WiLDAF

Mkurugenzi wa shirika la makazi la WAT-HST Judith Sando akifuatilia ripoti ya hali za haki za Wanawake iliyoandaliwa na WiLDAF

Mh Anne Makinda katika maadhimisho ya siku ya wanawake wa Afrika iliyoandaliwa na WiLDAF

Wafanyakazi wa WiLDAF Jacqueline na Alicko wakifuatilia mada katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika yaliyoandaliwa na WiLDAF

Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt Judith Odunga na Mgeni rasmi Mh Anne makinda wakifuatilia mada katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Africa yaliyoandaliwa na WiLDAF

Washiriki toka mashirika mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa afrika yaliyoandaliwa na WiLDAF

Mh Anne Makinda na Mwenyekiti wa bodi ya WiLDAF katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika

Baadhi ya wafanyakazi wa WiLDAF katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika.